Kiswahili

Kujitoa Kikamilifu!

Agosti 19, 2022
Ijumaa ya Wiki ya Ishirini ya Kipindi cha Kawaida
Masomo ya Leo

Mtakatifu Yohane Eudes, Padri—Kumbukumbu ya Hiari

Video

Sikiliza kwa Kiingereza

Mafarisayo waliposikia kwamba Yesu alikuwa amewanyamazisha Masadukayo, walikusanyika pamoja, na mmoja wao, mtaalamu wa sheria, akamjaribu kwa kumuuliza, “Mwalimu, ni amri ipi katika sheria iliyo kuu kuliko zote?” Akamwambia, “Mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.”  Mathayo 22:34-37

“Kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.”  Yaani, kwa nafsi yako nzima!

Upendo wenye kina hiki unaonekanaje katika maisha ya kila siku?  Ni rahisi jambo hili kubaki kuwa wazo la hali ya juu au mahubiri ya maneno tu, lakini ni changamoto kulifanya wazo hili au mahubiri haya kuwa ushuhuda unaoonekana katika matendo yetu.  Je, unampenda Mungu kwa nafsi yako nzima?  Kwa kila sehemu ya utu wako?  Hilo linamaanisha nini hasa?

Huenda upendo wenye kina hiki ukajidhihirisha kwa njia nyingi; hizi hapa ni baadhi ya sifa zitakazokuwapo katika upendo huu:

1) Kujikabidhi: Kuyakabidhi maisha yetu kwa Mungu ni sharti la upendo.  Mungu ni mkamilifu na, kwa hiyo, kumpenda kunahitaji kwamba tuuone ukamilifu Wake, tuuelewe ukamilifu huu, na tutende kulingana nao.  Tunapoona na kuelewa Mungu ni nani, matokeo yake ni kwamba hatuna budi kumtumainia kikamilifu na bila kujibakiza.  Mungu ni mwenyezi na mwenye upendo usio na kikomo.  Mungu mwenyezi na mwenye upendo usio na kikomo hana budi kutumainiwa bila kikomo.

2) Moto wa ndani: Kujikabidhi kwa Mungu kutawasha moto mioyoni mwetu!  Hii ina maana kwamba tutamwona Roho Mtakatifu akifanya mambo ya ajabu ndani ya roho zetu.  Tutamwona Mungu akitenda na kutubadilisha.  Hayo yatakuwa makubwa kuliko chochote ambacho tungeweza kujifanyia wenyewe.  Mungu ataongoza na kufanya mambo makuu ndani yetu, akiyabadilisha maisha yetu, kama vile moto mkali unavyoteketeza kila kitu.

3) Matendo yanayozidi uwezo wako: Matokeo ya moto mkali wa Roho Mtakatifu ndani yetu ni kwamba Mungu atafanya mambo makuu kupitia sisi katika maisha ya wale wanaotuzunguka.  Tutamshuhudia Mungu akitenda na kushangazwa na yale anayofanya.  Tutajionea wenyewe nguvu Zake za ajabu na upendo Wake unaobadilisha maisha, na hayo yatatendeka kupitia sisi.  Ni zawadi iliyoje!

Tafakari leo kuhusu kumpenda Mungu kwa nafsi yako nzima.  Je, umejitoa kikamilifu?  Je, umejitoa kabisa kumtumikia Bwana wetu na kutimiza mapenzi Yake matakatifu?  Usisite.  Inastahili!

Bwana, nisaidie kukupenda kwa moyo wangu wote, akili yangu yote, roho yangu yote na nguvu zangu zote.  Nisaidie kukupenda kwa nafsi yangu yote.  Katika upendo huo, ninakuomba unibadilishe niwe chombo cha neema Yako.  Yesu, nakutumainia!

Novena kwa Mtakatifu Monika
Agosti 18–26

Tafakari Zaidi za Injili

Tafakari juu ya Huruma ya Mungu

Watakatifu/Sikukuu Zote

Mtakatifu wa Siku – Mtakatifu Yohane Eudes, Padri

Machaguo ya Masomo ya Misa Takatifu

Picha Iliyoangaziwa: Mafarisayo na Masadukayo Waja Kumjaribu Yesu, na James Tissot, kupitia Wikimedia Commons