Jumapili, 10 Februari 2019
Jumapili ya Tano ya Kipindi cha Mwaka, Mwaka C
Mtakatifu Skolastika, Bikira â Kumbukumbu

Sikiliza kwa Kiingereza
âPelekeni mashua kwenye maji ya kina kirefu, mkashushe nyavu zenu ili kuvua samaki.â Luka 5:4
Inavutia kutambua kwamba Yesu hakuwaambia tu Petro na Mitume wapeleke mashua majini; bali aliwaambia waipeleke kwenye âmaji ya kina kirefu.â Jambo hili lina maana kubwa.
Mwishoni mwa mwaka mkuu wa jubilei wa 2000, Mtakatifu Papa Yohane Paulo II aliandika waraka wa kitume, Novo Millennio Ineunte ambao aliufungua kwa kunukuu kifungu hiki cha Injili. Kifungu hiki kiliweka mwelekeo wa waraka wake wote uliobaki, ambamo alitoa wito wa uinjilishaji mpya kwa milenia iliyokuwa inakuja.
âPelekeni mashua kwenye maji ya kina kirefu!â Tunapaswa kujifunza nini kutokana na maneno haya? Tunapaswa kumsikia Yesu akituambia nini? Tunapaswa kumsikia akituita âkushusha nyavu zetuâ bila kuchoka na kwa kujitolea, ili kuwavuta wengine wengi kwenye Injili. Petro na Mitume walipofanya hivyo wakiwa mashuani, walivua samaki wengi sana hata nyavu zao zikaanza kuchanika, nao wakastaajabu sana. Hiki ni kitendo cha kinabii tulichopewa ili kutuambia kwamba lazima tuinjilishe kwa shauku na ari kubwa kabisa, tukiwatafuta kondoo wa Mungu waliopotea kila mahali, mbali na karibu.
Ulimwengu tunamoishi unaweza kuwa na ukatili nyakati fulani. Watu wengi sana wamepotea na wamechanganyikiwa. Dhambi imeenea sana, na kukata tamaa kumetawala. Ulimwengu wetu unamhitaji sana Mwokozi, nasi ndio ambao Yesu anatamani kuwatumia ili kuvua samaki wengi na kuwapata wale wenye uhitaji mkubwa zaidi. Yesu alitaka Mitume wavue samaki waliokuwa kwenye maji ya kina kirefu kama njia ya kusema kwamba kuna roho zisizohesabika katika ulimwengu wetu zilizo mbali na Mungu. Kuna watu wengi âwanaoogeleaâ katika bahari ya kuchanganyikiwa na maumivu. Ni watu hawa hasa ambao Yesu anataka kuwavuta kwake. Ni wajibu wetu kuitii amri ya Bwana wetu na kwenda kuwatafuta.
Tafakari leo maneno haya ya Yesu: âPelekeni mashua kwenye maji ya kina kirefu.â Yesu anakuomba ufanye hivi kwa namna gani? Anakuitaje utoke katika hali uliyoizoea ya raha na usalama na âkushusha nyavu zako?â Anataka nini kutoka kwako, na anatamani kukutumiaje kuendeleza utume wa uinjilishaji. Itii amri Yake, nawe pia utastaajabia matunda mema yatakayozaliwa!
Bwana, ninatamani kujitoa Kwako ili nikutumikie na kukutukuza. Ninatamani kwenda kwa amri Yako, nikizitafuta roho zinazohitaji zaidi huruma Yako tele. Unipe neema ninayohitaji ili niwe mwaminifu kwa wito ulionipa, kusudi huruma Yako yenye upendo iwafikie wale wanaoihitaji zaidi. Yesu, nakutumainia.
Tafakari juu ya Huruma ya Mungu
Mtakatifu wa Siku – Mtakatifu Skolastika



