Kiswahili

Upendo kwa Mwenye Dhambi

15 Novemba 2022
Jumanne ya Juma la Thelathini na Tatu la Kipindi cha Mwaka
Masomo ya Leo

Mtakatifu Alberto Mkuu, Askofu na Mwalimu wa Kanisa—Kumbukumbu ya Hiari

Video

Sikiliza kwa Kiingereza

“Zakayo, shuka upesi, kwa maana leo lazima nikae nyumbani mwako.”  Luka 19:5b

Zakayo alikuwa na furaha iliyoje alipopokea mwaliko huu kutoka kwa Bwana wetu!  Kuna mambo matatu ya kuzingatia katika tukio hili la kukutana kwao.

Kwanza, watu wengi walimwona Zakayo kuwa mwenye dhambi.  Alikuwa mtoza ushuru na, kwa hiyo, hakuheshimiwa na watu.  Bila shaka hali hii ingemwathiri Zakayo na kuwa kishawishi kwake kujiona hastahili huruma ya Yesu.  Lakini Yesu alikuja hasa kwa ajili ya mwenye dhambi.  Kwa hiyo, ukweli usemwe, Zakayo ndiye aliyefaa kabisa kuwa “mpokeaji” wa rehema na huruma ya Yesu.

Pili, Zakayo alipoona kwamba Yesu alikuwa amemjia na kumchagua yeye kati ya wote waliokuwapo ili akae naye, alijawa na furaha!  Hali hiyo inapaswa kuwa hivyo pia kwetu.  Yesu anatuchagua kweli, na kwa hakika anataka kuwa pamoja nasi.  Tukijiruhusu kutambua hili, kwa kawaida matokeo yake yatakuwa furaha.  Je, unafurahi kwa kujua hili?

Tatu, kutokana na huruma ya Yesu, Zakayo alibadili maisha yake.  Alijitolea kuwapa maskini nusu ya mali yake na kumrudishia mara nne kila mtu aliyekuwa amemdanganya hapo awali.  Hii ni ishara kwamba Zakayo alianza kugundua utajiri wa kweli.  Alianza mara moja kuwarudishia wengine wema na huruma alizoonyeshwa na Yesu.

Tafakari leo juu ya Zakayo na ujione katika hali yake.  Wewe pia ni mwenye dhambi.  Lakini huruma ya Mungu ina nguvu kubwa zaidi kuliko dhambi yoyote.  Acha msamaha Wake wa upendo na jinsi anavyokukubali viwe na nguvu zaidi kuliko hisia zozote za hatia unazoweza kuwa nazo.  Na uruhusu zawadi ya huruma Yake izae rehema na huruma kwa wengine katika maisha yako mwenyewe.

Bwana mwenye upendo mkuu sana, ninakuelekea katika hali yangu ya dhambi na kuomba huruma na rehema Zako.  Nakushukuru mapema kwa kunimiminia huruma Yako.  Na niipokee huruma hiyo kwa furaha kuu, nami pia niwamiminie wengine huruma Yako.  Yesu, nakutumainia.

Jaribu programu yetu ya simu!

Tafakari Zaidi za Injili

Tafakari juu ya Huruma ya Mungu

Watakatifu/Sikukuu Zote

Mtakatifu wa Leo – Mtakatifu Alberto Mkuu, Askofu na Mwalimu wa Kanisa

Machaguo ya Masomo ya Misa Takatifu

Picha kuu hapo juu: Zakayo Juu ya Mkuyu Akimngojea Yesu Apite, iliyochorwa na James Tissot