Kiswahili

Sala Yenye Nguvu Kubwa Sana

Jumamosi, Oktoba 7, 2017

Masomo ya Kumbukumbu ya Mama Yetu wa Rozari

Mama Yetu wa Rozari – Kumbukumbu

Tunapomheshimu Mama Yetu wa Rozari leo, tuna nafasi nzuri ya kutafakari sala hii yenye nguvu. Njia bora ya kutafakari nguvu ya Rozari ni kuwasikiliza watakatifu. Hapa chini utapata kauli kadhaa za watakatifu wa Mungu kuhusu Rozari. Zitafakari na uziache zizungumze na moyo wako.

“Kamwe mtu anayesali Rozari yake kila siku hatapotoshwa. Hii ni kauli ambayo ningetia sahihi kwa damu yangu kwa furaha.” – Mtakatifu Ludoviko de Montfort.

“Kati ya sala zote, Rozari ndiyo nzuri zaidi na yenye utajiri mkubwa zaidi wa neema…ipende Rozari na uisali kila siku kwa ibada.” – Mtakatifu Pio X.

“Ni nzuri namna gani familia inayosali Rozari kila jioni.” – Mtakatifu Papa Yohane Paulo II.

“Rozari ndiyo sala ninayoipenda zaidi. Ni sala ya ajabu! Ni ya ajabu kwa urahisi wake na kina chake.” – Mtakatifu Papa Yohane Paulo II.

“Rozari ni hazina isiyokadirika thamani, iliyotokana na uvuvio wa Mungu.” – ya Mtakatifu Ludoviko de Montfort.

“Hakuna njia ya hakika zaidi ya kuomba baraka za Mungu zishuke juu ya familia… kuliko kusali Rozari kila siku.” – Papa Pio XII.

“Rozari ndiyo namna bora kabisa ya sala na njia yenye ufanisi mkubwa zaidi ya kufikia uzima wa milele. Ni dawa ya maovu yetu yote, mzizi wa baraka zetu zote. Hakuna njia bora zaidi ya kusali.” – Mtakatifu Papa Leo XIII.

“Nipeni jeshi linalosali Rozari nami nitauteka ulimwengu.” – Mwenye Heri Papa Pio IX.

“Ikiwa mnatamani amani mioyoni mwenu, katika nyumba zenu, na katika nchi yenu, kusanyikeni kila jioni kusali Rozari. Msiiache hata siku moja ipite bila kuisali, hata mkiwa mmelemewa namna gani na mahangaiko na kazi nyingi.” – ya Papa Pio XI.

“Mama Yetu hajawahi kuninyima neema niliyoiomba kwa kusali Rozari.” – ya Mtakatifu Padre Pio wa Pietrelcina.

“Njia bora kabisa ya kusali ni kusali Rozari.” – Mtakatifu Fransisko wa Sales.

“Siku moja, kwa njia ya Rozari na Skapulari, Mama Yetu atauokoa ulimwengu.” – Mtakatifu Dominiko.

Bwana, nijalie kuelewa nguvu ya zawadi hii ya thamani, Rozari Takatifu. Nipe neema ya kuifanya iwe sehemu ya sala yangu ya kila siku. Yesu, nakutumainia.

Zaidi>>>


  Subscribe to our YouTube channel  
  to be notified about new content.